MECHI YA BONGO DANSI NA WATANASHATI WA MUJINI HAKUNA MBABE …Kalala Jr, Abraham Chove, Julius Kihampa waacha gumzo



MECHI YA BONGO DANSI NA WATANASHATI WA MUJINI HAKUNA MBABE …Kalala Jr, Abraham Chove, Julius Kihampa waacha gumzo

Mechi ya kuimarisha udugu iliyojaa vibweka vya kila aina kati ya Bongo Dansi na Watanashati wa Mujini, ilimalizika kwa sare ya 0-0 kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam Jumapili jioni.

Bongo Dansi inayoundwa na wanamuziki na wadau wa muziki wa dansi, ikakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Watanashati wa Mujini ambao kama si uimara wa kipa wa Bongo Dansi Abraham Chove basi wangeweza kuibuka na ushindi.

Hamis Dacota, Majuto Omar, Kalala Jr, Muhidin Sufiani, Jose Mara, Hamza Mapande, Chiki Mchoma na Nassoro Chambuso ni miongoni tu mwa sura zilizoiopamba timu ya Bongo Dansi huku Watanashati wa Mujini wakitesa zaidi na MC Double A, Amon, Gara B na Julius Kihampa ambaye alikuwa ndio nyota wa mchezo kwa upande wa timu yake.

Hakuna ubishi kuwa nyota wa mchezo kwa upande wa Bongo Dansi alikuwa ni Kalala Jr ambaye alizungusha sentahafu ya kufa mtu.

 



Comments