MASHABIKI WA KLABU YA LIVERPOOL WALIVYOFIKISHA UJUMBE WAO KUPINGA KUPANDA KWA BEI ZA TIKETI ZA KLABU YAO



MASHABIKI WA KLABU YA LIVERPOOL WALIVYOFIKISHA UJUMBE WAO KUPINGA KUPANDA KWA BEI ZA TIKETI ZA KLABU YAO
Mashabiki wa klabu ya Liverpool siku ya jana waliutumia mwanya walioupata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya timu ya Stoke City kwa kupeperusha bango kubwa lilionesha kutoridhika kwao kwa kitendo cha kupandishiwa bei ya tiketi kwenye michezo ya klabu hiyo.
Mashabiki hao walilionesha bango hilo lililoonesha namna ambavyo bei ya tiketi kwa klabu yao imekua ikipanda kwa ghafla tangu mwaka wa 1990 mpaka kufikia hivi sasa.

Kwenye bango hilo mashabiki hao walionesha kuwa bei ya tiketi ya kuwashuhudia majogoo hao wa Anfield ilikua paundi 4 mnamo mwaka 1990, ambayo ilipanda mpaka kufikia kiasi cha paundi 24 mnamo mwaka 2000 na sasa ghalama hiyo imepanda mpaka kufikia kiasi cha paundi 43 mnamo mwaka 2010 mpaka sasa.


Comments