 KLABU ya Manchester United imeichapa          mabao 3-0 Hull City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni          ya leo Uwanja wa Old Trafford.
KLABU ya Manchester United imeichapa          mabao 3-0 Hull City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni          ya leo Uwanja wa Old Trafford.Mabao          ya United yamefungwa na Chris
        Smalling          dakika ya 16, Wayne Rooney dakika ya 42 na Robin van Persie          dakika ya 66.
        United          ilipata pigo baada ya winga wake, Angel di Maria kutolewa nje          dakika ya 14 baada ya kuumia, nafasi yake ikichukuliwa na          Ander Herrera.
        Katika          mechi nyingine, Liverpool imeilaza 1-0 Stoke City bao pekee la          Glen Johnson, West Ham imeifunga 1-0 Newcastle bao la          Aaron Cresswell, wakati Swansea imetoka 1-1 na
        Crystal          Palace na QPR imeilaza 3-2 Leicester, Burnley ikitoka 1-1 na          Aston Villa.
        Mchezo          uliotangulia jioni ya leo, Arsenal
        imeichapa          1-0 West Brom bao pekee la Danny Welbeck.
         
  
 
Comments
Post a Comment