Imedaiwa kuwa Mchezaji mholanzi anaekipiga klabuni Manchester united Daley Blind (pichani) hatokaa nje ya uwanja kwa miezi 6 kama ilivyodaiwa awali
Mchezaji huyo anayesaidia kuimarisha safu ya kiungo ya klabu hiyo aliumia mwishon mwa juma lililopita katika pambano la kimataifa la taifa lake dhidi ya Latvia ambalo walishinda 6-0
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, umemnukuu kocha wa klabu hiyo Louis van Gaal akisema "anahitaji kupumzika kwa siku kumi kasha baada ya hapo ndo tutajua" akaongeza "siwezi kusema itakuwa wiki sita, ama nane, wala siwezi kusema itakuwa wiki kumi ama kumi na mbile ila hakika haitokuwa miezi sita.
Ikumbukwe, mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo mwenye miaka 24 alisajiliwa kwa dau la paundi £13.8m kutoka klabu ya Ajax ya uholanzi katika dirisha la kiangazi mwaka huu na amekuwa msaada mkubwa katika nafasi ya kiungo ya klabu hiyo.
Comments
Post a Comment