MANCHESTER UNITED WATALIPA £785,000 WIKI HII KWA WACHEZAJI MAJERUHI



Screen Shot 2014-11-22 at 5.46.26 PMManchester United watatumia kiasi cha £785,000 wiki hii kulipa mishahara ya wachezaji ambao ni majeruhi na wale walio na mashaka ya afya zao wakati timu ikielekea Emirates jioni ya leo kwenda kukipiga na Arsenal.

Kikosi cha Louis van Gaal kimekuwa kikiandamwa na majeruhi kila mara na haijalishi kama wachezaji wake wapo fiti au majeruhi klabu hiyo hiyo bado inatoa mamilioni kila wiki kulipa mishahara ya wachezaji.

Mmoja wa wachezaji wanaolipwa vizuri sana na bado wapo majeruhi ni mshambuliaji wa Colombia Radamel Falcao, huku Van Gaal akithibitisha kwamba mshambuliaji huyo atakuwa nje ya uwanja wa wiki mbili baada ya kupata majeruhi kwenye misuli.
Falcao, ambaye yupo United kwa mkopo kutoka Monaco, anavuna kiasi cha £280,000 kwa wiki – kwa maana hiyo mshambuliaji tangu awasili Old Trafford ameshavuna kiasi cha £4m huku amecheza mechi 5 tu, akitoa assists mbili na kufunga goli moja.
Daley Blind atakuwa nje kwa miezi kadhaa baada ya kuumia goti, lakini mchezaji huyo bado atakuwa akivuta kiasi cha  £75,000 kila wiki.

Mlinzi Marcos Rojo, ambaye analipwa £70,000 kwa wiki nae ameumia bega katika mchezo dhidi ya Manchester City. Atakuwa nje kwa wiki kadhaa zijazo.

Rafael, anayevuna £50,000 kwa wiki, ana tatizo la misuli, Jones (£50,000-a-week) nae yupo nje kwa wiki kadhaa sasa, wakati Evans (£65,000-a-week) ana majeruhi ya enka.

Katika safu ya kiungo,  Ashley Young, ambaye hupeleka nyumbani kila wiki mshahara wa  £115,000 ana maumivu ya groin lakini anategemea kurudi dimbani hivi karibuni.
Michael Carrick, ambaye anavuna £80,000 kwa wiki, alipata majeruhi ya misuli wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya England lakini anatarajiwa kurudi dimbani hivi karibuni.



Comments