Man Utd wanajipanga kwa golikipa wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen kuchukua nafasi ya David De Ge?
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 22 aliyehamia Nou Camp kutoka Borussia Monchengladbach ya ujerumani kwa karibu ya kitata cha £ 10million katika dirisha la majira ya joto, lakini ameshindwa kuonyesha makali yake chini ya kocha Luis Enrique.
Ter Stegen bado hajapangwa kwenye ligi ya hispania( La Liga ) msimu huu, na Claudio Bravo ndiyo chaguo la kwanza kwenye miamba mitatu, lakini amepangwa mara nne kwenye Ligi ya Mabingwa.
Na ripoti kutoka Hispania zinadai kwamba kipa huyo wa kimataifa wa ujerumani anatarajia kuihama timu hiyo katika dirisha dogo la usajili la januari, na United ndiyo inaonekana kuwa ndiyo sehem anayoweza kuhamia .
Red Devils shot-stopper De Gea ameandaliwa kiasi kikubwa cha pesa na Real Madrid, na United inaweza kugeukia kwa Ter Stegen kama kipa wao wa kwanza ataondoka kwenda Santiago Bernabeu
Comments
Post a Comment