MAN CITY YAFANYA KWELI YAICHAPA SOUTHAMPTON 3-0



MAN CITY YAFANYA KWELI YAICHAPA SOUTHAMPTON 3-0
LICHA ya kucheza pungufu baada ya Eliaquim Mangala kutolewa kwa kadi nyekundu, Manchester City imepata ushindi mnono ugenini wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu ya
England jioni ya leo.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa St Mary's, Yaya Toure aliifungia bao la kanza City dakika ya 51, kabla ya Mangala kutolewa kwa kadi ya pili ya njano dakika ya 74.

Pamoja na kubaki wachache, mabingwa hao watetezi walifanikiwa kuongeza mabao kupitia kwa Frank Lampard aliyetokea benchi dakika ya 80 na Gael Clichy dakika ya 88.

Beki Vincent Kompany alitolewa nje dakika za mwishoni baada ya kuumia, lakini City haikubadili mchezaji kwa kuwa ilikwishamaliza nafasi baada ya James Milner, Lampard na Martin Demichelis wote kutokea benchi
kuchukua nafasi za Stevan Jovetic, Samir Nasri na Jesus Navas.



Comments