MAMA SAKINA WA MASHUJAA BAND AHUDHURIA SHOW YA TWANGA PEPETA …Bongo Dansi na Watanashati wa Mujini wasababisha




MAMA SAKINA WA MASHUJAA BAND AHUDHURIA SHOW YA TWANGA PEPETA …Bongo Dansi na Watanashati wa Mujini wasababisha
MAMA SAKINA WA MASHUJAA BAND AHUDHURIA SHOW YA TWANGA            PEPETA …Bongo Dansi na Watanashati wa Mujini wasababisha

Moja ya malengo ya mechi ya Bongo Dansi na Watanashati wa Mujini iliyofanyika Jumapili Leaders Club, ilikuwa ni kuimarisha udugu na ndivyo ilivyokuwa.

Mkurugenzi wa kamapuni ya Mashujaa Group inayomiliki Mashujaa Band, Sakina Mbange maarufu kama Mamaa Sakina, alihudhuria mechi hiyo na baadae kushuhudia onyesho la bendi pinzani – Twanga Pepeta.

Kwa zaidi ya miaka miwili, wamiliki wa bendi hizo mbili (Mamaa Sakina wa Mashujaa na Asha Baraka wa Twanga Pepeta) ambao ni maswahiba wakubwa, hawajawahi kutembeleana kwenye bendi zao kutokana na namna bendi hizo zilivyoibuka kuwa na ushindani pamoja na uhasama wa kibiashara.

Ushindani na kuchukuliana wanamuziki, ukafanya wawili hao waweke uswahiba kando, lakini mechi ya jana ya Bongo Dansi na Watanashati wa Mujini ikavunja mwiko na hatimaye Mamaa Sakina akashuhudia onyesho la Twanga Pepeta.

Saluti5 ikamshuhudia Mamaa Sakina ambaye ni mwanachama wa makundi yote hayo mawili, akikaa Leaders hadi majira ya saa 1.30 za jioni. Hongereri sana Bongo Dansi na Watashati wa Mujini kwa hatua hii.

Pichani juu kushoto ni Mamaa Sakina akifutialia onyesho la Twanga. Kulia ni mwandishi wa habari Esther Bhoke Mbussi  wa New Habari.



Comments