Luiz Adriano tayari amefanikiwa kufikia rekodi ya ufungaji mabao ya Cristiano Ronaldo katika ligi ya mabingwa Ulaya. Mbrazil huyo ambaye aliitwa katika kikosi cha timu ya Taifa, mwezi huu amefunga mabao tisa katika katika michezo mitano ya hatua ya makundi na na endapo atafunga katika mchezo wa mwisho wakati klabu yake ya Shaktar Donestks itakapocheza na FC Porto, Disemba 10 atakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya michuano hiyo kufunga mabao zaidi ya tisa katika michezo ya hatua ya makundi, rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na Ronaldo.
Katika orodha hiyo ya wafungaji bora msimu huu, Leonel Messi ndiye anayemfuatia Mbrazil huyo. Messi amefunga mabao saba anashika nafasi ya pili. Sergio Aguero, Karim Benzema, Edsons Cavanni na Jackson Martinez wote wamefunga mabao matano matano. Cavanni alifunga mara mbili katika ushindi wa mabao 3-1 wa PSG dhidi ya Ajax Amsterdam. Martinez mshambulizi raia wa Colombia alifunga moja ya mabao matatu ya Porto katika ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya BATE Borisov.
Kiungo-mshambulizi wa zamani wa Manchester United, Luis Nani alifunga bao lake la nne katika michuano hiyo msimu huu na kuisaidia timu yake ya Sporting Lisbon kuishinda NK Maribor kwa mabao 3-1 na kusogea hadi katika nafasi ya pili nyuma ya Chelsea na juu ya Schalke 04. Nani ambaye anacheza kwa mkopo amefunga mabao manne sambamba na kiungoo wa klabu yake, Yacine Brahimi.
Cristiano Ronaldo, Klans Jan Huntelaar, Adriano Ramos, Yao Gervinho, Danny Welbeck, Seydou Doumba, Alex Teixeira, Pieere Aubameyang, Cillo Immobile wte hawa wafunga mabao matatu matatu. Je, Adriano anaweza kuweka rekdi mpya ya ufungaji katika hatua ya makundi na kufunga mabao 10 au zaidi? Ni jambo la kusubiri na kuona.
Comments
Post a Comment