LIONEL MESSI WA BARCELONA NA REKODI ZAKE, SABABU MUHIMU YA YEYE KUENDELEA KUBAKI ‘LA LIGA’



LIONEL MESSI WA BARCELONA NA REKODI ZAKE, SABABU MUHIMU YA YEYE KUENDELEA KUBAKI 'LA LIGA'

sisiKatika moja ya simulizi zake mwandishi mashuhuri James Hadley Chase kupitia kitabu chake cha the "The Joker In The Pack" anajaribu kueleza namna mwanadamu anavyoweza kufanikiwa au kukwama katika harakati zake mbalimbali sababu ya uwepo wa 'Joka katika pakiti la Karata".

Mwandishi huyu anafananisha harakati mbalimbali za mwanadamu na mchezo wa karata ambapo mtu anarusha kete zake, anatumia mbinu zake na mara anapokaribia kushinda mchezaji mwingine anaokota "Joka" ambayo yaweza kuwa kete muhimu kwa mhusika au la.

Ndivyo unavyoweza kuelezea Messi katika jezi ya barcelona na rekodi zake. Binafsi, naitizama kama sababu tosha ya yeye kusalia 'Camp nou'. Ni wiki sasa gumzo katika mitandao limekua messi kuihama Barcelona.
Inawezekana kukawa na sababu, pengine kushuka kwa kiwango cha barcelona iloogopwa ulaya, pengine sababu ya kuchezeshwa mahala asipopapenda (Luis Enirique anamtumia zaidi kama mchezeshaji "Playmaker") au pengine yaweza kuwa kuisha kwa hamu ya mafanikio kama anavyodai gwiji mwingine mashuhuri wa klabu hiyo Mario Kempesi. Haijalishi sababu ipi ina mashiko zaidi bado ila Messi anaihitaji barcelona kama Joka iliaendelee kutamba na kutamba.

Usiku wa kuamkia jana, messi amefanikiwa kuandika rekodi muhimu katika ligi kuu ya hispania, almaarufu 'la liga' na hivyo akiifikia na kuipiku rekod ilowekwa na Telmo zarra mnamo mwaka 1955.

sisi 1

Ikumbukwe, wakati Telmo Zarra anafariki mwezi februari mnamo mwaka 2006, Leo alikuwa ndo kwanza yuko katika msimu wake wa pili kwenye la liga akiwa na goli saba tu. Hata hivyo baada ya miaka nane messi kaifikia rekodi hiyo, ajabu!
Akiwa na miaka 27 natamani kumuona akifunga na kufunga zaidi ili kuboresha rekod zake kuliko kuziacha kwa namna ambazo zinaweza kupitwa na wachezaji wengine, hususani mpinzani wake katika kizazi hiki, cristiano Ronaldo huku pengine akihaha kuendana na mfumo wa klabu atayohamia, mbaya zaidi unaeza kuhamia klabu nyingine ukaharibu kabisa awatizame kina Ronaldinho na Kaka

bado natamani kumuona akifunga na kufunga kama ambavyo telmo zarrra mshambuliaji wa zaman wa Athletic Club angetamani kumuona mshambuliaji mahiri huyu. Na pengine atatusaidia kuendelea kuwaonesha vizazi vya kale vyenye kuamini hakuna wachezaji wa kulinganisha na akina "Pele, Maradona, George Best, Di Stefano, Puskas na wengineo"

Sahau msimu wa 2006-07 alipowakimbiza mabeki wa Getafe katika kombe la mfalme na kufunga bao kama la maradona kwa waingereza mwaka 2006, bado la liga imempa mengi ambayo hapaswi kuyakimbia

sisi 2
ni wiki chache tu ameifikia rekod ya Rauli Gonzalenz UEFA akiwa na Barcelona, Barcelona imempa goli nying zaidi kombe la mfalme kuliko mchezaji yoyote, Barcelona imempa goli nyingi zaidi katika pambano la jadi almaarufu "El classico", barceelona imempa magoli mengi zaidi katika klabu hiyo kuliko mchezaji mwingine yeyote, imempa tuzo ya Ballon d' or mara 4 mfululizo!!!! Kama ningekuwa na fursa ya kumwona walau ningemnong'oneza 'Barcelona ni joka kaka baki hata kama huna furaha'.



Comments