KIEMBA AIBUKIA MAZOEZINI AZAM FC


KIEMBA AIBUKIA MAZOEZINI AZAM FC

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kiungo mkongwe wa simba SC Amri Kiemba leo asubuhi ameibuka katika mazoezi ya Azam FC yaliyoanza baada ya mapumziko ya wiki mbili kujiandaa kwa mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Yanga SC itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 28, mwaka huu.
Kuibuka mazoezini kwa Kiemba kunakuja ikiwa ni siku mbili tu baada ya Simba SC kutangaza kupitia kwa msemaji wake Hamphrey Nyasio kumpeleka Aza FC kwa mkopo kiungo huyo aliyekuwa amesimamisha kwa madai ya utovu wa nidhamu na kucheza chini ya kiwango awamo klabuni msimbazi.

kiemba
Kiemba, kiungo mpya wa Simba SC, Shaban Kisiga na winga Haroun Chanongo walisimamishwa na uongozi wa klabu hiyo muda mfupi baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya Oktoba 25, mwaka huu na kumriwa kurejea jijini Dar es Salaam kwa mahojiano zaidi.
Kisiga alisamehewa baada ya kukiri makosa na kuomba radhi lakini Kiemba na Chanongo walibaki kwenye hali ya 'moshi mweusi.'
Azam FC walipeleka dili ya kumtaka kwa mkopo kiungo huyo anayefanya vizuri akiwa na Taifa Stars lakini Simba SC walikataa ofa hiyo wakitaka Azam FC imnunue moja kwa moja badala ya kumtaka kwa mkopo vingine wapewe beki Said Morad ambaye ni wazi hatakuwa na namba katika kikosi cha kwanza cha Mcaeroon Joseph Omog baada ya kusajiliwa kwa beki kisiki Serge Wawa kutoka El-Marreikh ya Ligi Kuu ya Sudan.



Comments