Na Andrew Chale
        ASIA Idarous Khamsin na                Safari  Carnival  wanakuletea usiku wa Khanga Party na                Spice Modern Taarab watakaowasha moto wa burudani sambamba                na gwiji wa mipasho nchini Khadija Kopa pamoja na Bilal                Mashauzi,  Jumamosi ya usiku wa Novemba 29, ndan ya ukumbi                wa Safari Carnival, Mikocheni B.
        Kwa mujibu wa  mmoja wa                wandaaji wa usiku huo, Asia Idarous Khamsin,  amesema                tayari maandalizi yake yamekamilika na amewasihi wadau                kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo la aina yake  kwa                kiingilio cha sh 10,000 na 20,000 kwa V.I.P.
        Asia Idarous Khamsin                alisema Usiku wa Khanga, itaanza kuanzia usiku wa saa                mbili  na kuendelea huku vazi maalum likiwa ni Khanga.
        "Usiku huu ni maalum                kulienzi vazi la khanga, ambalo pia ndilo vazi maalum la                usiku huo. Pia watafurahia muziki mzuri kutoka kwa magwiji                wa taarab hapa nchini akiwemo Khadija Kopa, Spice Modern                taaba na Bilal Mashauzi." alisema Asia Idarous Khamisin                 ambapo pia alisisitiza vazi la khanga ni la heshima hasa                kwa mwanamke wa Kitanzania hivyo kila mmoja                atakapolitengeneza vizuri ama kufunga litamweka malidadi.
        Aidha, alibainisha kuwa,                usiku huo pia kutakuwa na  zulia jekundu 'Red Carpet'                ambapo watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa na                watu maalufu watakao jitokeza usiku huo.
        Pia alibainisha kuwa,                tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali jijini Dar                es Salaam ikiwemo Fabak fashions Mikocheni na Safari                Carnival  kwa mawasiliano piga 0754263363 au 0713263363
        
Comments
Post a Comment