KAWEMBA CEO MPYA AZAM FC



KAWEMBA CEO MPYA AZAM FC

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
UKISEMA wa nini, wenzio wanasema watampata lini! Baada ya kushindwa kukubalika katika uongozi mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliyekuwa mkurugenzi wa mashindano wa shirikisho hilo, Saad Kawemba ameajiriwa kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Azam FC.
Kawemba, aliyeng'ara katika uongozi wa aliyekuwa rais wa TFF, Leodegar Tenga, hakupewa mkataba mpya na uongozi mpya wa TFF chini ya Rais wake Jamal Malinzi baada ya mkataba wake kumalizika Desemba mwaka jana licha ya kuligharimu Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) mamilioni ya shilingi katika kumwongeza ujuzi wa masuala ya utawala wa soka.

saa

Mwenyekiti wa Azam FC, Said Muhammad amemtambulisha rasmi leo Kawemba mbele ya wachezaji na viongozi wa Azam FC kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam, baada ya mazoezi ya asubuhi.
"Nafurahi kupata nafasi hii, ni fursa nyingine tena ya kupata uzoefu mwingine katika uongozi wa soka baada ya kufanya kazi kwa mafanikio TFF," Kawemba amesema baada ya kutambulishwa jana.
Muhammad amesema Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC imefikia hatua ya kuajiri Mtendaji Mkuu ili kurahisisha uendeshaji ndani ya klabu kwa lengo la kutafuta ufanisi zaidi.
Kawemba amesema anatarajia kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani.
"Nimekuja hapa kusaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo la Azam FC, ninatarajia ushirikiano wa wote,"amesema.



Comments