Kala Jeremiah kaja na kitu kingine kipya, Usikate tamaa akiwa amemshirikisha Nuruwell, kwa kweli kazi hii imeongeza ukomavu wa Kal ambaye kama zilivyopitz tungo zake nyingine toka mara ya kwanza alipoonekana kwenye BSS, ameweza kupanga mistari ikawa inafurahisha kusikiliza na yenye ujumbe mzito. La ziada katika kazi hii ni arrangement ya muziki uliosindikiza ujumbe, imekuwa na ukomavu na hata kuingiza zeze la kiasili kwa mbali hapa na pale kumeweza kuiboresha kazi hii. Hongera Kala kwa mara nyingine. Video pia ni kazi nzuri sana inayostahili kupongezwa
Comments
Post a Comment