Na Mwandishi wetu,Mara.
KIKUNDI cha Wanaume wapiga kasia cha JJ Buda kutoka Nyarusurya Mkoani Mara kimeibuka na ubingwa katika fainali za Mkoa za mashindano yambio za mitumbwi chini ya udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager zijulikazo kama "Balimi Boat Race 2014" na hivyo kikundi hicho kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na kuwakilisha Mkoa wa Kagera kwenye fainali za Kanda zinazotarajiwa kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Benedict Chamba ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Tumaini Maendeka kutoka Kisorya ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Bernard Charles kutoka Nyarusurya ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=
Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni Siagi Siagikutoka Kinesi, Chuma Musa kutoka Kinesi, Matiku Nkoba kutoka Kuruya, Paul Mwita kutoka Nyarusurya, Ostadhi Magori Kutoka Kuruya na Emmanue Jemes kutoka Resti
Upande wa Wanawake kikundi cha Nyamizi Deokutoka Kisorya kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini Mwanza.
Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi cha Maria Sarige ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindi wa tatu ni kikundi cha Edina Peterkutoka Bwai ambao walizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Rosalina Johanes kutoka Nyarusurya ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Khadija Simon kutoka Nyarusurya, Debora Malima kutoka Bweri, Winfrida Majinge kutoka Bukabwa, Tatu Siagi kutoka Kinesi, Justina Kambarage kutoka Kinesi, na Siwema Doto kutoka Majengo.
Jumla ya vikundi 90 vilijitokeza kushiliki mbio hizo za makasia chini ya udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Meneja matukio wa wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela aliwashukuru wakazi wa Mara kwa kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ambapo pia aliwapongeza walishinda na kupata nafasi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za Kanda Desemba 6, Mwaka huu na kuwaomba ambao hawakufanikiwa wakajipange kwa mwaka ujao.
Fainali za Kanda za mbio za mitumbwi zijulikanazo kama "Balimi Boat Race 2014" zinatarajiwa kufanyika Desemba 6, mwaka huu jijini Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.
Comments
Post a Comment