MWINJUMA Muumin "Kocha wa Dunia" jana akiwa na kundi zima la G Five Modern Taarab, alijitosa studio kurekodi wimbo wake mpya wa taarab "Jasho la Baba".
Muumin mwimbaji mkali wa muziki wa dansi, amerekodi wimbo huo katika studio za Sound Crafters Temeke jijini Dar es Salaam.
Hii inakuwa ni kete ya pili ya Muumin katika muziki wa taarab, kete yake ya kwanza ilikuwa ni wimbo wa "Kigodoro" uliotoka miezi kadhaa iliyopita.
Mkurugenzi wa G Five Modern Taarab, Hamis Slim ameiambia Saluti5 kuwa matarajio ni wimbo huo kuanza kusikika mwishoni wa wiki hii.
Comments
Post a Comment