Paul Gascoigne Gazza amefunguka kwamba klabu ya Arsenal kwa          ujumla ililipa kiasi cha £50,000 ambayo ni zaidi ya millioni 100          ya Kitanzania kwa ajili ya matibabu – na sehemu kubwa ya fedha          hiyo ilitolewa na kocha Arsene Wenger.
          Gazza, 47, alionekana mitaani kwa mara ya kwanza hivi karibuni          baada ya kupelekwa kwenye kituo cha magonjwa ya akili baada ya          kushamiri kwa tabia yake ya ulevi wa kupindukia mwezi uliopita.
          Kiungo huyo zamani wa England ameadithia, namna Arsenal klabu          ambayo hakuwahi kuichezea walivymsaidia katika kulipia matibabu yake.
'Nilimpigia daktari wa Arsenal Gary Lewin na nikamwambia kwamba sikuwa najisikia vyema. Akaniambia niende hosptali kwa sababu alihofia ni pneumonia. Wenger akakubali kulipa kiasi cha £28,000 kulipia matibabu yangu. Arsenal kama klabu ikatoa kiasi cha £22,000 nilipokuwa nafanyiwa upasuaji wa hips.'
Lakini, wakati Spurs ilipokuwa ikicheza na Real Madrid katika          Champions League aliambiwa na klabu yake ya zamani kwamba          itabidi alipe ili kuingia uwanja wa White Hart Lane.
          'Nilitaka kuangalia mchezo wa Spurs vs Madrid na nikaishia          kuambiwa kwamba walikuwa na tiketi 2 tu za £60. Nilipaswa kwenda          kukaa kwenye sehemu ya watu maalum lakini nikaishiwa kuambiwa          nilipe."
Gazza kwa sasa aemrudi kwenye afya yake na ameahidi kujirekebisha.
Comments
Post a Comment