EXTRA BONGO YAANIKA WASANII WAKE WAPYA, YAANZA RASMI KAMBI, KUREJEA JUKWAANI DISEMBA 20


EXTRA BONGO YAANIKA WASANII WAKE WAPYA, YAANZA RASMI KAMBI, KUREJEA JUKWAANI DISEMBA 20

BENDI ya Muziki wa dansi ya Extra bongo Next Level Wazee wa Kizigo imeingia kambini rasmi kujipanga na ujio wake mpya ambapo jana iliwatambulisha wanamuziki wapya kutoka Congo DRC.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  bendi hiyo, Ally Choki, alisema, baada ya kimya cha takribani miezi miwili kufuatia msiba wa mkewe Mama Shuu sasa wanarejea rasmi jukwaani.

Alisema Extra Bongo imeongeza nguvu kwa kuwachukua wapiga magitaa watatu kutoka  DRC ili kuimarisha safu yao ya wapiga vyombo.

Aliwataja wanamuziki hao kuwa ni Ornely Malongi, Carlos Cardinal na Mairlaiw Mpian.

Choki, alisema, baada ya kukaa kambini kwa wiki nne bendi hiyo itaanza rasimi maonyesho yake Desemba 20 mwaka huu katika ukumbi wa Meeda wakizindikizwa na vikundi mbalimbali burudani..

Wakijipanga kwa ujio huo tayari wamemrudisha kundini  kundini mpiga kinanda maarufu nchini Thabiti Abdul na kuongeza wapiga vyombo watatu kutoka nchini Congo C

 "Kimya chetu cha muda mrefu kitazimwa na shoo maalum tuliyoiandaa na hatujaishia hapo kuongeza wanamuziki kwani kunawanamuziki wengine watatu wanatarajia kutua wakitokea nchini Congo," alisema.

 Kutoka ni Juma Kasesa, Nyamwela na Ally Chocky

 Safu ya washambuliaji wa Exxtra Bongo ikifanya vitu vyake mbele ya waandishi wa habari

Kutoka kulia ni Ornely Malongi, Carlos Cardinal



Comments