DEKULA KAHANGA VUMBI KATIKA VIDEO MPYA YA WIMBO LIVERPOOL




DEKULA KAHANGA VUMBI KATIKA VIDEO MPYA YA WIMBO LIVERPOOL

F8B1107

Dekula Kanga Vumbi safari hii kaja na kibao kinaitwa Liverpool, wimbo huu ni wa aina yake sana hasa katika siku hizi ambazo katika muziki wa rumba, gitaa la rythm limeshushwa sana thamani katika arrangement. Vumbi ameweza kupiga wimbo huu kwa dakika nne za mwanzo akitumia vyombo vitatu tu, drums, gitaa la bezi na gitaa la rhythm na gitaa hilo ndilo likiwa linaongoza wimbo huo. Katika sekunde hamsini za mwisho ndipo lilipoingizwa solo gitaa na mwendo kuongezwa kwa mtindo wa sebene. Uimbaji mzuri kabisa unavutia kusikiliza wimbo huu. Watu kadhaa ambao muhimu katika historia ya muziki wa Tanzania  wametajwa akiwemo marehemu Anko Julius Nyaisanga. Pia utamu mwingine uliomo ni kibwagizo cha 'Kachiri kachiri mume wangu kasafiri….' kibwagizo kilichopata umaarufu katika wimbo wa Kilimanjaro Band 'Kachiri' ulioimbwa na Mabruk Khamis maarufu Babu Njenje. Asante vumbi kwa kibao hiki, hili gitaa la rhythm linaleta hamu kusikiliza tena na tena wimbo huu wa Liverpool. Katika wimbo huu pia katajwa Michuzi ambaye ni mpenzi anayejulikana wa Liverpool



Comments