Tayari makundi ya michuano ya Copa America yamepangwa, na sasa yaonyesha kwamba, miamba wa soka wa America ya kusini Brazil watakuwa na kibarua na wapinzani wao katika robo fainali iliyopita ya kombe la dunia, Colombia..katika hatua ya makundi…
Miamba hawa watakutana kwenye kundi la C, ambalo pia lina nchi za Peru na Venezuela, huku miamba wengine wa bara hilo Argentina,wakiwa sambamba na mabingwa watetezi wa taji, Uruguay, Paraguay pamoja na Jamaica katika kundi la B, kwenye michuano hiyo ya mwaka 2015.
Kwenye kundi la A, hili linaongozwa na wenyeji wa michuano Chile, wakiwa sambamba na nchi za Mexico, Ecuador na Bolivia, kujumuisha timu jumla ya 12, katika michuano itakayoanza jijini Santiago kuanzia Alkhamis, ya June 11, mwaka ujao.
Brazil ilikutana na Colombia kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia iliyofanyika mwaka huu kwenye nchi hiyo, na kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja, mechi ambayo ilishuhudia staa wake Neymar akiumia, na akilazimika kukosa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Pamoja na hivyo kuna vitu vingi vya kukumbuka hapa, na kuwekwa wazi, kama vile suala la Staa wa klabu ya Barcelona ya Hispania, aliyenunuliwa kwa ada ya pauni milioni 75, Luis Suarez, …Staa huyu atakosa michuano hii..
Sababu kubwa za kukosa michuano hii mikubwa kwa Suarez, ni tukio lake la kufungiwa mechi tisa za kimashindano, rungu alilopewa na mamlaka kuu za soka la dunia Fifa, kutokana na kitendo chake cha kumuuma beki wa Italia, Giorgio Chiellini, kwenye mechi za fainali za kombe la dunia.
Kwenye kundi ambalo wapo wanafainali wa kombe la dunia wa mwaka huu Argentina, kutakuwa na ule mchezo wa Re Final ya mwaka 2011, baina ya Uruguay dhidi ya Paraguay,huku Reggae boyz wa Jamaica wakiwa miongoni mwao kama waalikwa, ambao wanaalikwa kama ilivyo kwa Mexico.
Kikanuni, michuano hii mikubwa ya Copa America, timu mbili za juu zitafuzu kwa hatua inayofuata sambamba na timu mbili zitakazofuzu kama best Looser, ambazo zitacheza hatua ya robo fainali, kuelekea fainali itakayopigwa mnamo Julai 4.
Comments
Post a Comment