COAST MODERN TAARAB KUPAGAWISHA MSATA


COAST MODERN TAARAB KUPAGAWISHA MSATA
Na Mwandishi Wetu, Kibaha
BENDI ya Muziki wa Taarabu ya Coast Modern Taarab ya Jijini Dar es Salaam inatarajia kutoa burudani Novemba 27 mwaka huu kwenye mji wa Msata wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha mkurugenzi wa ukumbi itakapofanyika onyesho hilo, Msukuma Pub Msukuma Mwinzarubi alisema kuwa maandalizi yamekamilika.
Mwinzarubi alisema kuwa burudani hiyo itaongozwa na gwiji wa taarabu Jokha Kassim ambaye anatamba na kibao chake cha Domo la Udaku.
"Burudani itakuwa ya uhakika kama mnavyoijua Coast Medern Taarab wanavyopagawisha mashabiki wa muziki huu ambao unapendwa kwa sasa," alisema Mwinzarubi.
Alisema kuwa wapenzi wa muziki huo wa wilaya ya Bagamoyo na maeneo mengine wategemee burudani nzuri na ya kuvutia.
"Pia kutakuwa na burudani mbalimbali za muziki za wasanii wa Msata wakiwemo Wasafi Group na wasanii wengine ili kusindikiza burudani ambayo itatolewa siku hiyo," alisema Mwinzarubi.
Aidha alisema kuwa lengo la burudani hiyo ni kuzindua vyombo vya muziki ambavyo viliharibika kutokana na ajali ya gari ambalo lilibeba vyombo hivyo.


Comments