Chelsea imetoa onyo kali kwenye Ligi ya Mabingwa baada ya kuifumua Schalke ya Ujerumanj 5-0 katika mchezo wa kundi G na kujihakikishia kufuzu hatua ya 16 bora wakiwa kileleni.
Magoli ya Chelsea yalifungwa na Terry dakika ya 2, Willian 29, Kirchhoff (bao la kujifunga) 44, Drogba 76 na Ramires 78.
Mshambuliaji mkongwe Didier Drogba alizidi kudhihirisha kuwa bado fiti kwa kufunga bao moja na kutengeneza moja lililofungwa na Ramires.
Chelsea imefikisha pointi 11, nne zaidi kwa wanaoshikilia nafasi ya pili Sporting Lisbon.
Schalke inayofundishwa na kocha wa zamani wa Chelsea, Roberto Di Mateo, ilishindwa kabisa kufurukuta na kujikuta ikiruhusu karamu ya magoli.
Comments
Post a Comment