Mshambuliaji wa klabu ya League 1 ya nchini Ufaransa ya Bastia Brandao amepewa adhabu ya kifungo cha mwezi mmoja jela kufuatia kumtwanga kichwa kiungo wa klabu ya PSG, Thiago Motta, tukio lilotokea kwenye mchezo wa ligi hiyo.
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa, tayari amekwishakutana na adhabu nyingine, akipewa rungu la kuwa nje ya kabumbu kwa kipindi cha miezi sita kutokana na tukio hilo, kwenye mchezo ambao PSG iliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri mnamo August 16.
Kwa upande wake Motta, mwenye umri wa miaka 32, aliachwa akivunjika pua kutokana na tukio hilo la kushambuliaji na Brandao, ambae pia alitozwa faini ya pauni 15,850 ambazo ni sawa na Euro 20,000.
Hata hivyo, mwanasheria wa Brandao anasema alitarajia mshambuliaji huyo angepewa adhabu ya kuitumikia jamii, na si kuwekwa jela.
Brandao,ambae alishinda taji la ligi ya Ufaransa akiwa na klabu ya Olympique de Marseille msimu wa mwaka 2010, ametamka kwamba kiungo Motta alimtolea maneno ya kibaguzi ndani ya mchezo.
Kwa mujibu wa Motta akitoa ushahidi wake kwa polisi amesema kwamba, wakati Brandao akifanyiwa mabadiliko, alimwambia kuwa atamsubiri kwenye Korido lakini yeye hakutilia maanani, na ndipo alipomkuta na kukumbana na kadhia hiyo, akinaswa na kamera.
Nae raisi wa klabu ya PSG Nasser Al-Khelaifi akitoa maoni yake amesma kwamba, mshambuliaji Brandao alipaswa kufungiwa maisha kutokana na kitendo chake alichofanya.
Hii na ile ya Zizzou ni tofauti???
Comments
Post a Comment