Baba aibuka asema; ‘ Fellaini si mcheza rafu wa kimataifa’


Baba aibuka asema; ' Fellaini si mcheza rafu wa kimataifa'

Marouane-FellainiAbdellatif Fellaini ambaye ni baba mzazi wa kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Ubelgiji, Marouane Fellaini amewajibu wale wote ambao wamekuwa wakimuandama mwanaye kutokana na mchezo wake. Abdellatif amesema kuwa kuna uzushi mkubwa kuhusu Fellaini na amefikia kutamka maneno mazito katika vyombo vya habari hasa vile ambavyo vimekuwa vikiripoti kuwa, Fellaini hana faida.

" Kamwe mwanangu si mtu wa kujeruhi wenzake kwa makusudi. Wanamwita ' mcheza rafu wa kimataifa', lakini yeye ni mchezaji kama walivyo wachezaji wengine. Kila mmoja anafahamu kwamba ni mchezaji mzuri. Suala la majeruhi lina wakati wake na lazima likufike" alisema, Abdellatif.

Fellaini amekuwa akishutumiwa na vyombo vya habari vya Uingereza kwamba amekuwa akicheza soka la ubabe na kuwaumiza wenzake kwa makusudi, jambo ambalo limepingwa vikali na baba yake na kusema ni madai ya kipuuzi.

Fellaini alimchezea vibaya kiungo Joe Allen wa Wales wakati Ubelgiji ilipokutana timu hiyo kutoka Visiwa vya Uingereza wiki hii katika mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Ulaya, 2016, Ufaransa.

"Alimpiga kichwa usoni mpaka akatoka damu puani, lakini hakuna hatua ambazo mwamuzi alizichukua. Wakati mwingine waamuzi wana tabia ya kuwabeba wachezaji wakorofi," liliandika gazeti la Sports Daily la England kuhusu tukio la kiungo huyo wa Manchester United ambalo alilifanya dhidi ya Joe wa Liverpool.

 



Comments