Mlinzi wa zamani wa kutumainiwa wa Klabu ya Liverpool, Jamie Carragher amesema klabu yake hiyo ya zamani inatatizo la uongozi na ndio sababu imekua dhaifu na hivyo kuambulia vichapo mfululizo. Mchezaji huyo ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa habari za michezo ameeleza hayo ikiwa ni muda mfupi tu tangu majogoo hao wa Anfield walipoambulia kichapo toka kwa klabu ya Crystal Palace mapema jana.
Timu hiyo ambayo nusura iutwae ubingwa wa ligi hiyo msimu uliopita ikajikuta imeishia nafasi ya pili, imekua katika kiwango dhaifu hivi karibuni tofauti na matazamio ya wengi. Mfano, mpaka sasa klabu hiyo inashika nafasi ya 12, ikiwa na pointi nne tu zaidi ya zile zilizo kwenye msitari wa kushuka daraja. Ikiwa imecheza michezo 12 klabu hiyo imepoteza nusu ya mechi hizo.
Kwa upande mwingine Bosi wa klabu hiyo, Brendan Rodgers amekubali lawama zote kuelekezwa kwake kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo. Akizungumza na Sky Sport, Mlinzi Jamie Carragher amedokeza kuwa kuna tatizo la uongozi katika klabu hiyo na hivyo kupelekea makali ya timu yake hiyo kupungua kwa miezi kadhaa sasa.
Akizungumza na mtandao huo, mchambuzi huyo amesema "Nikiwa kama mshabiki wa klabu hii nimekuwa ni mwenye masikitiko sana, inasikitisha kuona timu yako ikiwa katika kiwango kibovu na hivyo kufungwa kirahisi, hii ni zaidi ya kuuanza msimu vibaya, kuna kitu kinakosekana, ni kama mwishoni mwa msimu uliopita walivyopoteza uwanjani hapa na tukasema hawako vizuri kimwili na kiakili, bado wako hivyo"
Akaongeza "hii kilichojitokeza uwanjani hapa si mara ya kwanza, kimekuepo kwa muda sasa na tumekuwa tukiishia kusema kuna wachezaji wapya ambao inabidi wazoee mazingira, hata hivyo siamini sana katika hilo". "Angalia Luis Suarez alivyoondoka kisha uitizame klabu iwapo uwanjani utagundua hakuna uongozi uwanjani, hii inachangia matokeo mabaya"
Mchezaji huyo wa zamani pia ameongeza kuwa si wakati tena wa kusema wachezaji wapya waliosajiliwa majira ya kiangazi wanahitaji kuendelea kuzoea mazingira bali ni wakati wao wa kudhihirisha kwanini walisajiliwa
"sikuwahi kuhama hama katika vilabu, na hivyo ni wazi kuwa wakati mwingine mchezaji wa kigeni anahitaji muda kuzoea ila nadhani umefika wakati wa kuona viwango vyao pasipo kujali hilo"
"Liverpool imekua dhaifu kiasi kwamba haifungwi tu sababu ya kiwango dhaifu bali imekuwa kama inaonewa sasa. Vilabu vimekua na imani hiyo na hata ukiwatizama wanavyocheza ni hali ambayo utaitegemea. Hata wanapofungwa huoni wakicheza kiushindani kwa ari tizama walivyocheza baada ya Palace kupata bao la kusawazisha"
"tulikua na msimu mzuri, awamu ilopita tukapoteza, timu iliruhusu magoli 50 na bado hutazamii kama hali hiyo imefanyiwa kazi, unapoitizama ni wazi utagundua klabu hii inahitaji wachezaji wanne mpaka watano hivi"
Kwa mujibu wa wabashiri mbalimbali wa mambo nchini humo, bosi wa Liverpool, Brendan Rodgers anatajwa kama mmoja wa mameneja wanaokalia kuti kavu kiasi cha kuhatarisha vibarua vyao sambamba na meneja wa Aston Villa's Paul Lambert na yule wa Queen Park Rangers Harry Redknapp
Kwa upande mwingine kiungo wa klabu hiyo ambaye ni naodha msaidizi Jordan Henderson ameisistiza kuwa Steven Gerrard bado ni muhimu si tu katika timu hiyo bali pia kwa Uingereza. Ikumbukwe mwishoni mwa msimu uliopita ndoto za klabu hiyo zilianza kuzimwa kwa kichapo toka kwa Chelsea kabla ya sare ya kustaajabisha kutoka kwa Crystal palace wakati huo ikionewa na Tony Pulis.
Comments
Post a Comment