BAO pekee la mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni hii Uwanja wa The Hawthorns.
Danny alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 59 akimalizia mpira uliopigwa na Santi Cazorla na sasa The Gunners inasogea nafasi ya nne kabla ya matokeo ya mechi nyingine za wikiendi hii.
Saido Berahino aligongesha mwamba dakika 10 za mwishoni katika harakati za kusaka bao la kusawazisha na sasa West Brom inafikisha mechi saba bila kushinda Hawthorns msimu huu, jambo ambalo lilifanya wazomewe na
mashabiki wao mwishoni mwa mchezo.
Kikosi cha West Brom kilikuwa: Foster,
Wisdom, Dawson, Lescott, Pocognoli/Gamboa dk74, Mulumbu/Anichebe dk65, Gardner, Dorrans, Sessegnon/Samaras dk76, Brunt na Berahino.
Arsenal: Martinez, Chambers, Mertesacker, Koscielny Monreal/Gibbs dk23, Ramsey, Flamini, Sanchez, Cazorla, Welbeck na Giroud/
Oxlade-Chamberlain dk78.
Comments
Post a Comment