Timu ya Abajalo ya Sinza jijini Dar es Salaam imefanikiwa          kukata tiketi ya fainali ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014          baada ya kuifunga Burudani FC ya Temeke mikoroshini mabao 3-1.          Mabao ya Abajalo kwenye mchezo huo yalifungwa na Idd Kulachi          'Kleberson' aliyefunga mabao mawili kati ya matatu.
          Mchezo huo wa nusu fainali ya pili ulipigwa kwenye uwanja          Bandari uliopo maeneo ya Tandika Mwembe Yanga.
          Kwa ushindi huo sasa Abajalo itacheza na Tabata FC kwenye          fainali itakayopigwa siku ya jumapili ya tarehe 30/11/2014 pale          pale kwenye uwanja wa Bandari,huku timu za Black Six ya Buguruni          na Burudani zikipambana kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa          tatu wa michuano hiyo iliyovutia mashabiki kibao mpaka          sasa,Bingwa mwa mashindano hayo atapata pesa taslim shilingi          milioni tano huku mshindi wa pili akipata milioni tatu na          mshindi wa tatu akiambulia shilingi milioni mbili.
Comments
Post a Comment