Timu ya Abajalo ya Sinza                jijini Dar es Salaam imefanikiwa kukata tiketi ya fainali                ya Dr Mwaka Sports Xtra NDONDO CUP 2014 baada ya kuifunga                Burudani FC ya Temeke mikoroshini mabao 3-1. Mabao ya                Abajalo kwenye mchezo huo yalifungwa na Idd Kulachi                'Kleberson' aliyefunga mabao mawili kati ya matatu. Mchezo                huo wa nusu fainali ya pili ulipigwa kwenye uwanja Bandari                uliopo maeneo ya Tandika Mwembe Yanga. Kwa ushindi huo                sasa Abajalo itacheza na Tabata FC kwenye fainali                itakayopigwa siku ya jumapili ya tarehe 30/11/2014 pale                pale kwenye uwanja wa Bandari,huku timu za Black Six ya                Buguruni na Burudani zikipambana kwenye mchezo wa                kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo iliyovutia                mashabiki kibao mpaka sasa,Bingwa mwa mashindano hayo                atapata pesa taslim shilingi milioni tano huku mshindi wa                pili akipata milioni tatu na mshindi wa tatu akiambulia                shilingi milioni mbili.  
  
  
  
  
  
  
  
  AJALO
AJALO
        
Comments
Post a Comment