Ally Lityawi,KAHAMA
          KATIKA kujiwinda na pambano la ligi kuu Tanzania Bara mwishoni          mwa juma hili dhidi ya Kagera Sugar, Dar es salaam Young African          jana imecheza mchezo wa kijipima nguvu dhidi ya Ambasador FC na          kufanikiwa kuibuna na ushindi wa bao 1 kwa 0 kwenye uwanja wa          halmashauri ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. 
Bao hilo pekee na la ushindi la Dar es salaam Young Africans limekwamishwa nyavuni na Said Bahanuzi katika dakika ya 44 baada ya kumalizia kazi nzuri ya Hamisi Kiiza.
 
          Pambano hilo lililoshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally          Rufunga aliyeambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga          Khamis Mgeja lilishuhudia Yanga wakiwa mbele kwa bao hilo moja          hadi mapumziko.
Kivutio kikubwa katika pambano hilo kilikuwa ni kitendo cha Kipa Juma Kaseja kumpatia soksi zake kijana mmoja muokota mipira uwanjani Ally Juma Kasagura ambaye alionyesha kumshabikia wakati filimbi ya mapumziko ilipopulizwa na kaseja kutoka uwanjani.
Aidha wakati wa mapumziko wachezaji wa Brazili wa Yanga ambao muda wote wa mchezo walikuwa katika basi lao,walishuka na kwenda katika benchi la timu yao na kuzusha tafrani kubwa ya mashabiki waliokuwa wakitaka kushikana nao mikono na kulazimika uongozi kuwaamuru kurejea katika gari ndipo hali ilipotulia.
Kabla ya pambano hilo Uongozi wa Dar Yanga African mnamo majira ya saa tatu asubuhi ulizindua tawi la klabu hiyo wilayani Kahama na kutoa Kadi kwa wanachama wapya.
Comments
Post a Comment