WALIOMUUA CAPTAIN WA BAFANABAFANA KUTAMBULIWA KITAALAM, MKEWE AELEZEA JINSI WALIVYOMPIGA RISASI HUKU AKIWA NA BUNDUKI YAKE KIUNONI..!
Polisi nchini Africa Kusini wameonesha nyuso zinazo            dhaniwa kuwa ni wauaji wa golikipa na kapteni wa timu ya taifa            Africa Kusini Bafana Bafana, Senzo Meyiwa.
          Meyiwa alipigwa risasi na kufa siku            ya jumapili wakati alipokuwa akikabiliana na wavamizi            waloingia nyumbani kwa mpenzi wake Kelly Khumalo ambaye ni            mwanamuziki na pia ni muigizaji,maziko ya Meyiwa yanatarajiwa            kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
          Kifo cha mwanasoka huyo kimeonesha            picha halisi ya kiwango cha uhalifu na matumizi mabaya ya            silaha nchini Africa Kusini.
          Africa kusini inatajwa kuwa moja ya            nchi zenye matukio makubwa ya uhali,na kiwango cha uhalifu            kinazidi kuongezeka siku hadi siku.
          Mwanzoni mwa mwezi huu mwanariadha            Oscar Pistorious alihukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la            kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake.
        
Comments
Post a Comment