Uongozi wa Pirates, na ule wa Chiefs waomba Soweto Derby iharishwe, kufutia msiba wa Meyiwa



Uongozi wa Pirates, na ule wa Chiefs waomba Soweto Derby iharishwe, kufutia msiba wa Meyiwa

kaizer Chiefs imeungana na Orlando Pirates kuitaka bodi ya ligi ya Afrika kusini kuahirisha mchezo wa wapinzani wa jadi huko Soweto.
Pambano baina ya kaizer Chiefs na Orlando Pirates ulipangwa kufanyika siku ya jumamosi , lakini kifo cha Senzo Meyiwa kilichotokea jana usiku kimeharibu ladha ya pambano hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari , mwenyekiti wa Pirates Dr Irvin Khozaamethibitisha juu ya timu yake kuomba pambano hilo liahirishwe.
Dr-Irvin-Khoza-Pirates_2769468
Tumeiandikia barua bodi ya PSL na SAFA leo asubuhi , tukitaka pambano letu na Kaizer Chiefs liahirishwe,.
Pia tuliongea na mwenzetu Mr Kaizer Motaung leo asubuhikabla hatujatuma barua.tulikubaliana nae.
Kama utawala ingetuwia vigum kuendelea na maandalizi juu ya mchezo wakati kuna msiba.
Tunasubiri majibu , inawa tunaamini litasikilizwa na bodi ya PSL.
Khoza ataondoka leo jijini Durban kwenda kuungana na familia ya Meyiwa.



Comments