Tegete hapaswi kuondoka Yanga wakati huu…….


Tegete hapaswi kuondoka Yanga wakati huu…….

Na Baraka Mbolembole

Masaa machache tangu baba yake Mzazi aliposema hadharani kuwa mshambulizi, Jeryson ' Jerry' Tegete anapaswa kuachana na Yanga SC na kujiunga na Simba SC ili kunusuru kipaji chake, mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania alitumia dakika 18 kufunga mabao mawili na kuisaidia timu yake ya Yanga kuchomoza na ushindi wa mabao 3-0 wakicheza ugenini dhidi ya Stand United katika uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga.

" Jerry ni mchezaji mwenye kipaji cha kufunga mabao, nimemwambia mara kadhaa anapaswa kuondoka Yanga ikiwezekana akaenda Simba ili kunusuru kipaji chake" alinukuliwa akisema, John Tegete, baba wa mchezaji huyo. Akitokea benchi katika dakika ya 72 kuchukua nafasi ya Geilson Santos ' Jaja', Tegete,25 alifunga bao lake la kwanza akiwa ndani ya eneo la hatari akimalizia pasi ya Hussein Javu. Dakika ya mwisho ya mchezo alifunga ' bao la stahili yake' akimalizia mpira uliokuwa ' ukizagaa, zagaa' ndani ya eneo la hatari la Stand United. Tegete ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha kufunga mabao.

Wakati mwingine ushahuri wa ' mzazi' huwa ni jambo zuri lakini kwa mtazamo wa soka la Tanzania, bado Tegete anapaswa kumpuuza mzazi wake na kucheza soka ndani ya Yanga. Jerry bao ana muda mrefu wa kucheza mpira wa ushindani hilo pia lazima litazamwe kwa jicho la kimpira. Mzee Tegete amesema kuwa nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga kwa Jerry ni ' finyu' kutokana na uwepo wa mshambulizi, Geilsin Santos ' Jaja' lakini hakuna sababu ya msingi ambayo inaweza kumfanya Jerry kuondoka Yanga.

Juhudi zake, moyo wake, utayari wake, na moyo wa mchezaji mwenyewe ni kitu ambacho kinaweza kumfanya Jerry kurudi katika makali yake. Kitendo cha kufunga mabao mawili katika mchezo wake wa kwanza kinaweza kusukuma ' upya mwamko' na ' usongo' zaidi kwa mchezaji kuendelea kufanya vizuri. Nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga si rahisi kupata, lakini kama mcheza kama mchezaji mwenyewe atapambana jambo hilo ni rahisi.

Tegete ni mvumilivu, tangu aliposajiliwa na Yanga mwaka 2008 akitokea shule ya sekondari ya Makongo hawaja tayari kuondoka katika timu hiyo licha ya kuwa katika kipindi kigumu kwa miaka minne. Ushahuri mzuri kwa Jerry ni kuendelea kuwa mtulivu wakati huu ambao ' imani ya mashabiki' wa timu yake ikiwa ni ' 50,50'.. Kuna wachezaji wengi ambao wamepotea baada ya muda mfupi wa kucheza Yanga na Simba. Katika miaka ya karibuni kuna wachezaji kama, Rashid Gumbo ambae kupotea kwake kumetokana na uharaka wa kutaka kucheza Simba na Yanga ndani ya muda mfupi.

Unapohama timu kama Yanga na kujiunga na Simba, huwa ni kamari. Mwinyi Rajab na Mrundi mwenzake, Ramadhani Waso walikuwa wachezaji bora katika timu zao, Mwinyi wakati yupo Yanga na Waso wakati yupo Simba. Huwa hakuna urahisi wa moja kwa moja kwa mchezaji kupata mafanikio na wengi waliodiriki kufikia uamuzi huo hawakudumu. Tegete anaweza kucheza Yanga kwa miaka minne zaidi licha ya sasa kuonekana si mchezaji tishio. Anaendelea kukua, lakini atapotea kama ataenda Simba sehemu ambayo hatakuwa na ' nafasi ya moja kwa moja' katika kikosi cha kwanza kama ilivyo kwa Yanga, ni kupambana tu ndiko kunaweza kumrudisha zaidi Jerry katika makali yake wala si kuhamia Simba akiwa na umri wa miaka 25 sasa.

Akiwa na misimu sita sasa katika timu ya Yanga, Jerry ni mchezaji ambaye kipaji chake kipo wazi. Aendelee kucheza Yanga kwa muda zaidi huku akitazama mafanikio ya wachezaji kama Sekilo Chambua, Nadir Haroub, Fred Mbuna, ndiyo Mzee Tegete anataka, Jerry aende Simba lakini si chaguo zuri kwa sasa.

0714 08 43 08



Comments