Ron Gourlay, aachia ngazi Chelsea Football Club.



Ron Gourlay, aachia ngazi Chelsea Football Club.

GOGO

London, England

Ron Gourlay aliyekuwa mtendaji mkuu wa klabu ya Chelsea kwa kipindi cha miaka mitano ameachia nafasi hiyo ambayo aliirithi kutoka kwa Peter Kenyon.

" Klabu ya Chelsea inatangaza kwamba Ron Gourlay, baada ta miaka 10 ya mafanikio klabuni ikijumuisha miaka mitano kama Mtendaji Mkuu anaiacha Chelsea ili kuendelea na fursa mpya za kibishara"

"Klabu na hasa Mmiliki na Wakurugenzi, wanamshukuru Ron kwa miaka mingi ya huduma kwa Chelsea na tunamuunga mkono kwa hamu yake ya kutafuta changamoto mpya.

Juhudi za Ron zimeisaidia klabu kufanikiwa kwenye nafasi yake kama moja ya klabu kubwa duniani"

Kutokana na Gourlay kuachia ngazi mwenyekiti Bruce Buck na Mkurugenzi Marina Granovskaia wanatarajiwa kuongezewa majukumu zaidi ya kiutendaji mpaka hapo Mtendaji Mkuu mpya atakapoteuliwa.

Gourlay aliyejiunga na Chelsea mwaka 2004 na kufanya kazi kama Afisa Mtekelezaji Mkuu kabla ya kuchukua nafasi ya Peter Kenyon kama Mtendaji Mkuu mwaka 2009.

kabla ya kutua Chelsea, Gourlay aliwahi kufanya kazi Manchester United na kampuni ya Adiidas ambao ni watengenezaji wa vifaa vya michezo.

Ndani ya uongozi wa Gourlay Chelsea imeweza kunyakua kombe la ligi ya Uingereza, makombe mawili ya FA, Kombe la Europa na Kombe la klabu bingwa ya Ulaya lakini pia
alihusika kwenye mazungumzo ya kumrejesha kocha Jose Mourinho kwa mara ya pili kwenye klabu ya Chelsea.

Gourlay akitoa shukrani zake alisema "Nimekuwa na fursa ya pekee kufanya kazi kwenye klabu na kuwa na mafanikio nje na ndani ya uwanja kwa miaka 10, ila najiskia muda umefika kuendelea na changamoto zingine.

"Ningependa kumshukuru Mr Abramovich, Wakurugenzi, Meneja na wachezaji na wafanyakazi wengine wote kwa kuniunga mkono kwenye kipindi changu ndani ya klabu, nawatakia mafanikio zaidi"



Comments