RIO FERDINAD AFUNGIWA MECHI TATU, FAINI YA PAUNI 25,000 …kisa? kumtusi mtu kwenye ukurasa wa Twitter



RIO FERDINAD AFUNGIWA MECHI TATU, FAINI YA PAUNI 25,000 …kisa? kumtusi mtu kwenye ukurasa wa Twitter

Queens Park Rangers defender Rio Ferdinand has                    been given a three-game suspension by the FA

RIO Ferdinand nahodha wa zamani wa England amefungiwa mechi tatu pamoja na faini ya pauni 25,000 baada ya kumtusi mtu kwenye mtandao wa Twitter.

Beki huyo wa QPR alitumia neno "sket" kwenye maandishi yake, likiwa ni neno kutoka Caribbean likimaanisha mwanamke au msichana mwenye kulala na mabwana wengi.

Adhabu hiyo imetangazwa Jumatano na FA Jumatano, hiyo ikiwa ni baada ya kutiwa hatiani Oktoba 14.

Wakati wa siku ya mwisho ya usajili wa dirisha la kiangazi Septemba 1, mshabiki mmoja wa QPR aliandika: "Pengine QPR itasajili beki bora wa kati, wanahitaji kufanya hiyo", kauli hiyo ikamchafua Rio ambaye tayari alishasajiliwa QPR na akaona kama hilo ni dongo lake.

Rio akajibu: "Mlete mama yako aingie uwanjani kucheza #sket".



Comments