RAYMOND DOMENECH:-MOURINHO ANA MAPUNGUFU MAKUBWA



RAYMOND DOMENECH:-MOURINHO ANA MAPUNGUFU MAKUBWA

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Raymond Domenech amemwita Jose Mourinho "a translator" akimaanisha mwanafasiri wa Chelsea ambaye anamapungufu makubwa.

akiongea wakati wa uzinduzi wa kitabu chake kijulikanacho kama Mon dico passione du foot, chenye maana ya 'My Passionate Football Dictionary', kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 amewakosoa kwa kiasi kikubwa Nicolas Anelka, Franck Ribery pamoja na Zinedine Zidane.

RAY

tatizo kubwa la translators, Domenech akimaanisha Mourinho. "anajichanganya kiasi kikubwa kwa kauli zake mwenyewe."

mnamo August mwaka 2006, Mourinho alimlaumu Domenech kwa kumtumia Claude Makelele ambaye kipindi hicho alikuwa Chelsea kama mtumwa, Domenech alimtumia Makelele kwenye harakati za kufuzu michuano ya Euro mwaka 2008, japo kiungo huyo wa Ufaransa alikuwa nia ya kutaka kustaafu.

Domenech alilaumu kitendo cha Anelka, kufanya utovu wa ni dhamu kwenye timu ya taifa kitu kilichopelekea mshambuliaji huyo kurudishwa nyumbani kabla ya kumalizika kwa fainali za kombe la dunia mwaka 2010 Domenech, Anelka alijiona kila kitu kwenye timu kitu ambacho sio kweli.

Domenech pia alihoji tabia ya Ribery alioionesha kwenye fainali za kombe la dunia nchini Afrika kusini kitu kilichopelekea Ufaransa kumaliza michuano hiyo kwenye kundi A kwa kufungwa mchezo mmoja na kutoa sare michezo miwili,
Ribery aliifanya timu nzima ionekane ina tabia mbaya,
Kwa kufanya mambo yake ya kipumbavu , kule Afrika kusini, .lakini baada ya pale alibadilika na nadhani alijitambua kuwa anaweza kuwa mchezaji mkubwa kitu kitachomwezesha kutwaa tuzo ya Ballon d'Or.
Domenech kwenye kitabu chake amemwita Zinedine Zidane kuwa ni mtu mbinafsi na ubinafsi ndio uliopekea ampige kichwa Marco Materazzi kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka 2006 kitu kilichosababisha timu hiyo kukosa ubingwa.
Domenech amemsifia Thierry Henry kuwa ni mchezaji pekee ambaye alijitolea kwa kiasi kikubwa kuipa faida timu ya taifa ya Ufaransa akitolea mfano Henry alivyotoa pasi ya mkono na kuifanya timu hiyo ifuzu michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga timu ya taifa ya Jamuhuri ya Ireland mwaka 2009.



Comments