Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kesho (Oktoba 29 mwaka huu) anafungua kozi ya ukufunzi wa waamuzi ya FUTURO III ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
 Hafla ya ufunguzi wa kozi hiyo inayoshirikisha zaidi ya          waamuzi 40 wakiwemo baadhi ya wale ambao bado wanachezesha mpira          wa miguu kutoka nchi mbalimbali za Afrika itafanyika saa 4          asubuhi kwenye hoteli ya Holiday Inn, Dar es Salaam.
          
          Kati ya hao, washiriki wanane wa kozi hiyo inayoanza kesho hadi          Novemba 3 mwaka huu chini ya wakufunzi wa FIFA wakiongozwa na          Carlos Henriques ni kutoka Tanzania.
Washiriki kutoka Tanzania ni Emmanuel Chaula, Joan Minja, Josephat Bulali, Paschal Chiganga, Ramadhan Ibada, Richard Kayenze, Samuel Mpenzu na Soud Abdi.
Comments
Post a Comment