PICHA 8 TWANGA PEPETA: BUNDUKI MBILI ZIMEONDOKA, BUNDUKI MBILI ZIMEREJEA …Sabrina, Stella nje …Baby Tall, Ester ndani



PICHA 8 TWANGA PEPETA: BUNDUKI MBILI ZIMEONDOKA, BUNDUKI MBILI ZIMEREJEA …Sabrina, Stella nje …Baby Tall, Ester ndani
PICHA 8 TWANGA PEPETA: BUNDUKI MBILI ZIMEONDOKA, BUNDUKI            MBILI ZIMEREJEA …Sabrina, Stella nje …Baby Tall, Ester ndani

MADANSA wawili wa kike wa Twanga Pepeta wamepata ulaji wa kwenda kufanya kazi Dubai, huku madansa wengine wawili wa kike wakirejea nyumbani.

Sabrina Pazi na Stella George watakuwa nje ya jukwaa la Twanga kwa miezi mitatu kufuatia ulaji huo wa kwenda kunengua Dubai.

Lakini habari njema kwa Twanga ni kwamba wakati madansa hao wanaondoka, madansa wengine wawili wenye mvuto jukwaani, Ester na Baby Tall ambao walikuwa Dubai kikazi, wamerejea nyumbani na kuanzia wiki hii wataonekana kwenye majukwaa ya Twanga Pepeta.

Saluti5 imehabarishwa kuwa Ester aliyerejea wiki iliyopita, ameanza maozezi jana (Jumanne) wakati Baby Tall aliyereja jana mchana, atajumuika na wenzake mazoezini leo.

Madansa hao, wanatarajiwa kuanza kuonekana leo usiku katika onyesho la kila Jumatano pale Business Lounge – Machinga Complex Ilala nyuma ya Uwanja wa Karume.

Baby hapa akiwa njiani kurejea Bongo
Baby Tall kuanzia wiki hii atakuwepo kwenye majukwaa ya Twanga
Ester muda mfupi baada ya kutua Bongo
Ester atalipamba jukwaa la Twanga kuanzia wiki hii
 Sabrina hataonekana Twanga kwa miezi mitatu, yuko Dubai
Stela naye katimkia Dubai
Kushoto ni Ester na kulia ni Baby Tall
Stella (kushoto) akiwa na Sabrina

 



Comments