PICHA 15 ZA MWILI WA MDOGO WAKE ASHA BARAKA ULIVYOWASILI DAR JANA USIKU


PICHA 15 ZA MWILI WA MDOGO WAKE ASHA BARAKA ULIVYOWASILI DAR JANA USIKU
PICHA 15 ZA MWILI WA MDOGO WAKE ASHA BARAKA ULIVYOWASILI            DAR JANA USIKU

MWILI wa mdogo wake Asha Baraka, Bi Furaha Ramadhan Baraka aliyefia nchini Ubelgiji zaidi ya wiki moja iliyopita, uliwasili jijini Dar es Salaam jana usiku kama ilivyotarajiwa.

Mwili wa Bi Furaha ambaye amefuatana na Asha Baraka kwa kuzaliwa, uliondoka Brussels Ubelgiji juzi kwa Swiss Air na ukawasili Dar es Salaam Jumatano saa 2 usiku na baada ya taratibu zote, mwili ukachukuliwa na kwenda kuhifadhiwa nyumbani kwao Kinondoni Hananasif ambako ndipo msiba ulipo.

Mazishi yatafanyika leo saa 10 alasiri kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam na swala ya maiti itaswaliwa katika msikiti wa Maamur Upanda muda huo huo wa alasiri.

 

 Mwonekano wa sanduku lililobeba mwili wa marehemu mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege
 Sanduku lipo ndani ya gari tayari kwa safari ya Kinondoni
 Kutoka kushoto: Baraka Msilwa, Muddy Bawazir, Omar Baraka
 Mwili ukiwasili Kinondoni
 Ndugu na jamaa wakipokea mwili wa marehemu
 Huzuni na vilio
 Mwili unaingizwa ndani
 Asha Baraka (kushoto) akiwa hoi baada ya kuona sanduku lililobeba mwili wa mdogo wake
 Muddy Bawazir
 Simanzi imetawala
 Hamis Bwela
 Nyoso za huzuni
 Kutoka kushoto: Deo Mutta Mwanatanga, Hajj BSS, Miraj Shakashia, God Kanuti, Engi Muro Mwanamachame
Kutoka kushoto: Hajj BSS, Deo Mutta, Lilian Internet, Kaposhoo, Maria Saloma, Engi Muro

 



Comments