Paul Pogba ni wa Juventus hadi 2019


Paul Pogba ni wa Juventus hadi 2019

Mchezaji wa nafasi ya kiungo Paul Pogba amesaini mkataba mpya na klabu yake ya Juventus ya Italia. Makataba wa awali wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ulikuwa umalizike mwaka, 2016 lakini sasa nyota huyo alijiunga na Juventus miaka mitatu iliyopita akitokea Manchester United ya England atakuwa akilipwa kiasi cha pauni 70, 000 kwa wiki baada ya kusaini mkataba ambao utamfanya uwepo, Turin hadi mwaka 2019.
po

Pogba, 21 ametokea kuwa mchezaji bora wa nafasi ya kiungo barani Ulaya, ameshinda mataji mawili ya Serie A kwa sasa ni roho ya nafasi ya kiungo ya ' Bibi kizee wa Turin' akicheza sambamba na wakali, kama Andrea Pirlo, Claudio Marchisio na Artulo Vidal. Kocha Masimilliano Arlegi amefurahishwa na kitendo cha mchezaji huyo kusaini mkataba mpya ambao utambakiza klabuni hapo kwa muda mrefu.

pop

Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa mara kwa mara kuwa atsaondoka katika timu hiyo inayoshikilia ubingwa wa Italia kwa misimu mitatu mfululizo , klabu mbali mbali zimekuwa zikihusishwa kuhitaji huduma ya mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Ufaransa. Klabu yake ya zamani, United, Chelsea, mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich pia ni baadhi ya timu ambazo zilihusishwa na kutaka kumsaini mchezaji huyo chipukizi mwenye kipaji kikubwa.



Comments