PATA PICHA 5 ZA G FIVE WAKIWA STUDIO KUREKODI WIMBO WA ABDUL MISAMBANO



PATA PICHA 5 ZA G FIVE WAKIWA STUDIO KUREKODI WIMBO WA ABDUL MISAMBANO
PATA PICHA 5 ZA G FIVE WAKIWA STUDIO KUREKODI WIMBO WA            ABDUL MISAMBANO

KUNDI la G Five Modern Taarab, Alhamisi hii limeingia studio za Sound Crafters jijini Dar es Salaam kurekodi wimbo mpya utakaoimbwa na Abdul Misambano.

Wimbo huo unakwenda kwa jina la "Si mie ni moyo"  utunzi wake Misambano mwenyewe.

Ndani ya wimbo huo utakutana na kinanda kitamu cha Omar Kisila huku gitaa zito la bass likikung'utwa na Mussa Mipango.

Kweye gitaa linaloongoza (solo) kuna mkono wa Jumanne Ulaya.

Baada ya kutamba sana na wimbo wa "Asu" zaidi ya miaka 15 iliyopita, ujio mpya wa Misambano umekuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab.

Hiyo haimaanishi kuwa Misambano hajatoa nyimbo nyingine baada ya Asu, lakini ukweli ni kwamba hakuna wimbo wake uliopiku makali ya Asu.

Je "Si mie ni moyo" utaipiku Asu? Ni suala la kusubiri.

Omar Kisila akipapasa kinanda
Abdul Misambano akirekodi limbo wake "Si mie ni moyo"
Machiriku wa G Five wakifanya yao
 Kulia ni Mwamvita Shaibu na kushoto ni Aisha Kulele
Mkurugenzi wa G Five Hamis Slim akiwa na Abdul Misambano ndani studio za Sound Crafters

 



Comments