PATA PICHA 10 ZA ISHA MASHAUZI KWENYE TAMASHA LA SIKU YA MSANII MLIMANI CITY




PATA PICHA 10 ZA ISHA MASHAUZI KWENYE TAMASHA LA SIKU YA MSANII MLIMANI CITY
PATA PICHA 10 ZA ISHA MASHAUZI KWENYE TAMASHA LA SIKU YA            MSANII MLIMANI CITY

ISHA Mashauzi ambaye anashikilia taji la mwimbaji bora kike wa taarab kwa mujibu wa tuzo za Kili Tanzania Music Awards, Jumamosi iliyopita alidhihirisha ni kwanini alistahili tuzo hiyo.

Lakini Isha alionyesha pia ni kwanini alistahili tuzo ya mburudishaji bora wa kike ambayo nayo aliizoa miezi kadhaa iliyopita wakati tuzo za Kili zilipotolewa.

Isha alikuwa mmoja wa wasanii waliopewa ya kuburudisha kwenye tamasha la Siku ya Msanii lililofanyika Mlimani City Jumamosi iliyopita na akaitumia vema nafasi hiyo adhimu.

Akiwa msanii pekee wa taarab kuburudisha kwenye tamasha hilo, Isha akaangusha burudani safi iliyokidhi na kukonga nyoyo za watu waliofuruika ukumbini.

Pata picha 10.

 Alivyoonekana Isha na madansa wake
Isha akisukuma 'masauti' yake
Hapo ni mambo ya "Mapenzi Hayana Dhamana"
 Ilikuwa show tamu
 Mwendo wa kiduku sasa
 Waimbaji Zubeida, Naima na Asia walikuwa sambamba na Isha
Minenguo time
Wapigaji Rajab Kondo, Zaid na Kalikiti Moto wakifanya yao
 Burudani inaendelea
Kucheza wala haikuwa issue kwake, ilikuwa easy tu

 



Comments