Ndumbaro atoa ya moyoni aibua mambo mazito



Ndumbaro atoa ya moyoni aibua mambo mazito

ndumba

Mwanasheria Damas Ndumbaro amevunja ukimya kufuatia kifungo cha miaka saba alichopewa na Shirikisho la Soka Tanzania TFF akisema kamwe hawezi kuikubali huku akifichua ubadhilifu mkubwa wa fedha za wadhamini wa Taifa Stars.

Akizungumza jijini leo mara baada ya kurejea katika safari yake ya nchini Marekani Ndumbaro akitumia dakika 37 alisema ameshangazwa na hatua ya TFF kuamua kumfungia kifungo cha muda huo hali ya kuwa chombo hicho hakina mamlaka ya kumjadili kutokana na kazi yake ya kuhudumu sheria.

Ndumbaro alisema tayari ameshakata rufaa tangu Oktoba 21 kufuatia maamuzi hayo ambapo alisema kitendo cha shirikisho hilo kuchukua maamuzi hayo kinatokana na kiu ya uongozi wa TFF kutaka kufanywa wizi wa mchana kama ambavyo Naibu Waziri mpya,Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia aliwahi kutamka juu ya makato ya 5% za mgao wa fedha za wadhamini.

"Wakati klabu zinanipa kazi hii ikumbukwe kwamba hoja ya kunipa jukumu hilo iliotoka Yanga ambayo hapa TFF wanasema wanatilia shaka na kabla ya kukubali nilitaka klabu zote zikubaliane kimaandishi na wote wakasaini kasoro Stand United na hata Coastal Union walisaini kupitia makamu mwenyekiti wao,"alisema Ndumbaro.
ndumbaro
"TFF hawana mamlaka ya kunifungia nilikuwa pale nikitekeleza kazi yangu ya sheria kupitia kampuni yangu ya Maleta & Ndumbaro Advocate na sio kama Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba wala Mjumbe wa Bodi ya Ligi.

"Nakumbuka wakati tumekutana klabu, TFF na bodi ya ligi Naibu Wzairi Nkamia alitamka mbele ya kikao kile kwamba kitendo cha kutaka kuzikata klabu sh 100 katika kila tiketi huo ni wizi wa mchana sasa tafsiri ya adhabu hii ni sawa na kutaka kunyamazisha kwamba wizi wa mchana uendelee na sitokubaliana na hili nitazitetea klabu.

Aidha Ndumbaro alisema sababu kubwa ya TFF kulazimisha kwa nguvu makato hayo ni kutaka kuziba pengo la ubadhilifu mkubwa wa fedha za wadhamini wa Taifa Stars, Kilimanjaro, ambapo mpaka sasa kiasi cha Dola 159140 (shilingi 266 ml) ambazo zimeonekana kalipwa Rais wa TFF Jamal Malinzi

"Uchunguzi unaonyesha kwamba kiasi hicho cha fedha hakuna kielelezo kwamba zimekwenda kufanya nini sasa hawa jamaa walitumia siku mbili kunifungia lakini mimi tangu nimekata rufaa Oktoba 21 nikiwa Marekani mpaka siku kumi ninatimia hakuna kilichosikilizwa.



Comments