NDANDA FC YAWEKA REKODI VPL


NDANDA FC YAWEKA REKODI VPL

NDANDA

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KLABU ya Ndanda FC licha ya kufanya vibaya katika mechi za mwanzo wa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), imeweka rekodi katika ligi hiyo.
Rekodi ya kwanza ya timu hiyo yenye maskani yake Masasi, Mtwara, ni timu pekee iliyofunga goli katika mechji zote nne za kwanza msimu huu. Hakuna timu nyingine iliyofanikiwa kufunga goli katika mechi zote nne.
Pili, ni timu pekee iliyofungwa goli walau moja katika mechi zote nne za awali. Ndanda FC ilianza kwa kuishindilia Stand United mabao 4-1 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga kabla ya kufungwa 3-1 na Mtibwa Sugar, 2-1 na Coastal Union na 3-1 na Ruvu Shooting.
Nne, ni timu pekee iliyopoteza mechi nne mfululizo. Baada ya kufungwa 1-0 nyumbani na Mgambo Shooting katika mechi ya raundi ya tano.
Simba SC imeweka rekodi kwa kuwa timu pekee iliyotoka sare tano mfululizo katika mechi zote tano za awali msimu huu baada ya kutoka 2-2 na Coastal Union, 1-1 na Stand United, 1-1 na Polisi Morogoro, 0-0 na Yanga kabla ya sare ya 1-1 na Prisons iliyowafanya makocha wa timu hiyo wapewe sharti la kushinda mechi mbili zijazo dhidi ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting, vinginevyo watatimuliwa.



Comments