NAPOLI KUKETI KITAKO NA LIVERPOOL ILI KUMNASA BALOTELLI USAJILI WA JANUARI


NAPOLI KUKETI KITAKO NA LIVERPOOL ILI KUMNASA BALOTELLI USAJILI WA JANUARI

Balotelli is yet to score in the Premier League for                  Liverpool since joining from AC Milan in the summer

Napoli iko tayari kuanza mazungumzo na Liverpool kuhusu dili la kumsajili mshambuliaji anayeeelezwa kushuka kiwango, Mario Balotelli katika dirisha la usajili wa Januari.

 

Balotelli, ambaye amejiunga na the Reds kutoka AC Milan miezi mitatu iliyopita, amepokewa na wakati mgumu Anfield – akiwa hajaifungia bao timu hiyo katika mechi za Premier League.

Lakini wakati thamani yake ikishuka Merseyside, amebaki juu nyumbani kwao Italia, ambako ripoti zinasema kocha wa Napoli, Rafael Benitez yu tayari kutoa ofa ya pauni milioni 10 kumrekesha Balotelli katika Serie A mwezi Januari.

Liverpool inaelezwa haina tatizo na hasara watakayopata baada ya kuilipa Milan pauni milioni 16 kwani inaweza kutumia fedha watakayopata kuwekeza kwa ajili ya mshambuliaji Saido Berahino wa West Brom.



Comments