Nahodha ambaye pia ni golikipa wa timu ya soka ya taifa la Afrika kusini Senzo Meyiwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi. Jeshi la polisi la nchi hiyo limesema.Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika nyumba ya mpenzi wake iliyopo katika mji wa Vosloorus kusini mwa Johannesburg.
Mchezaji              huyo mwenye umri wa miaka 27 aliichezea klabu ya Orlando              Pirates na alicheza mechi nne zilizopita za timu yake ya              taifa katika mechi za kufuzu za fainali ya mataifa ya              Afrika.
        Jumamosi              alikuwepo katika tukio la timu yake pindi waliposonga mbele              katika nusu fainali ya ligi ya Afrika kusini.
        Katika              maelezo yake Jeshi la polisi la afrika kusini limesema              kwamba Meyiwa ameripotiwa kufariki wakati akiwasili              hospitalini.
        
Comments
Post a Comment