MwanaFA kuangusha bonge la shoo nyumbani Tanga



MwanaFA kuangusha bonge la shoo nyumbani Tanga
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn  Mworia(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati alipokuwa akizungumzia kuhusiana na shoo ya"Vodacom life is better"itakayofanywa na msanii wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA (kushoto)siku ya ijumaa katika klabu ya La Casachika mjini Tanga.Kulia ni Meneja wa msanii huyo Lusajo Mwaisaka.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya MwanaFA (kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na maandilizi ya shoo yake ya "Vodacom life is better"atakayoifanya siku ya ijumaa kwenye klabu ya La Casachika mjini Tanga,Anaeshuhudia katika ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia na kulia ni Meneja wa msanii huyo Lusajo Mwaisaka.


Wakazi wa Tanga wametakiwa kukaa mkao wa kula kwani  burudani ya nguvu ya muziki itapigwa moja kwa moja jukwaani siku ya tarehe 31 ya mwezi huu wa Oktoba katika ukumbi wa Lasachika mkoani humo.

Shoo hiyo ya kipekee na ya aina yake italetwa na si mwingine bali ni mkali wa muziki wa bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika ya Mashariki kwa vibao vyake mbalimbali si mwingine ni MwanaFA. Mwanamuziki huyo atafanya shoo laivu mkoani Tanga chini ya udhamini mkubwa wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania akisindikizwa na DJ Zero pamoja na mtangazaji wa Clouds FM B12.

Msanii MwanaFA mwenye mafanikio makubwa ya kimuziki wa kizazi kipya nchini amekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa ndani na nje ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali za muziki nchini. 

Akizungumzia juu ya shoo hiyo ya kukata na shoka kwa wakazi wa mkoa wa Tanga, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema Vodacom Tanzania wakiwa kama wadau namba moja wakuu wa kuinua tasnia hii ya muziki na michezo kwa ujumla wameamua kudhamini shoo ya "Vodacom Life is better"itayofanywa na MwanaFA  mkoani Tanga ikiwa ni sehemu ya burudani kwa wateja wao, kufurahi kwa pamoja na kuwashukuru kwa kuendelea kutumia huduma za kampuni hiyo."Hivyo ndivyo Vodacom tunafanya maisha ya wateja wetu kuwa murua".Alisema Mworia.

"Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano nchini." Alisema Mworia.

Kwa kuongezea Mworia amewaomba wakazi na mashabiki wote wa MwanaFA  na muziki wa Hip Hop  kujitokeza kwa wingi katika shoo hiyo iliyopewa jina la"Vodacom life is better show"kwani mbali na burudani kuwepo kutakuwepo na huduma na bidhaa mbali mbali za Vodacom. "Hivi ndivyo amabavyo Vodacom tunafanya maisha ya wateja wetu kuwa murua" alisema Mworia.

Naye MwanaFA alisema kwamba katika kunogesha  shoo yake hiyo ameamua kuambatana na DJ Zero ambaye atakuwa akifanya mambo yote kwenye jukwaa kwani ni mkali na anaijua kazi yake kwa hiyo shoo hiyo si ya kukosa kabisa kwani nimejipanga vya kutosha kuwaburudisha ndugu zangu wa nyumbani kwa hiyo uwepo wako tu pale utakufanya ujisikie vizuri kwani nitatenda haki kwenye shoo hiyo.Nawapenda sana wakazi wa Tanga na nipo tayari kuwaburudisha kama nifanyavyo sehemu zingine ndani nan je ya nchi.Alisema MwanaFA.


Comments