MRITHI WA ARSENE WENGER HUYU HAPA …ni kocha msaidizi wa Real Madrid


MRITHI WA ARSENE WENGER HUYU HAPA …ni kocha msaidizi wa Real Madrid

Paul Clement Rumoured as Eventual Arsene Wenger                  Replacement at Arsenal

GAZETI la The Sun limeandika kuwa kocha namba 2 wa Real Madrid, Paul Clement anaelezwa kuongoza orodha ya wanaopendekezwa na Bodi ya Arsenal kurithi mikoba ya Arsene Wenger mara Mfaransa huyo atakapoamua kuondoka Emirates.

Wenger amebakisha miaka miwili na nusu katika mkataba wake wa sasa, lakini anaweza kufunga virago mwisho wa msimu kama the Gunners itamaliza Premier League bila taji na kukosa moja kati ya nafasi nne za juu.

Clement, 42, amekuwa msaidizi wa Carlo Ancelotti wakati Mtaliano huyo akipata mafanikio Stamford Bridge, Paris Saint Germain na sasa Madrid, na anaelezwa kuwa mmoja kati ya makocha bora katika dunia ya soka.

Mwingereza huyo hajashika nafasi ya juu katika klabu yoyote, lakini asili yake ya kufanya kazi na baadhi ya nyota wa daraja la juu duniani wakati akiwa Ufaransa na Hispania inamuweka katika nafasi ya kupewa mikoba the Gunners.



Comments