MOROCCO; BAUSI NDIYE ALIKUWA TATIZO KWA NADIR, AGGREY NA SI ZFA



MOROCCO; BAUSI NDIYE ALIKUWA TATIZO KWA NADIR, AGGREY NA SI ZFA

MOROCO

Na Baraka Mbolembole,

Wakati akitoa sababu za kutowaita katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar, walinzi wa kati, nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub na kaimu nahodha wa Azam FC, Aggrey Morris ,; Salum Bausi aliyekuwa kocha wa Zanzibar Heroes alisema kuwa wachezaji hao wameadhibiwa na Chama cha soka cha Zanzibar kutokana na wachezaji hao kukataa kurudisha kiasi cha pesa ambacho wachezaji hao waliamua kugawana baada ya Zanzibar kushinda nafasi ya tatu michuano ya Challenge Cup iliyofanyika nchini Uganda mwishoni mwa mwaka 2012.

Wachezaji hao hao waligoma kurudisha sehemu ya dola 10,000 ambazo ni zawadi ya ushindi wa tatu katika michuano hiyo ya Mataifa ya Ukanda wa Cecafa; " Ni wachezaji bora ambao wanaweza kuisaidia Zanzibar katika michuano ijayo ya Challenge" anasema kocha wa timu hiyo, Hemed Morocco ambaye jana alitangaza orodha ya awali ya wachezaji 36 ambao watachujwa na kubaki wachezaji 20 kwa ajili ya michuano hiyo itakayoanza baadae mwezi ujao.

Nadir na Aggrey wameitwa kwa mara nyingine katika kikosi hicho ambacho kilifanya vibaya katika michuano ya mwaka jana nchini Kenya.; " Sina matatizo na wachezaji hao, ZFA pia walinihakikishia kuwa hawakuwa na matatizo na wachezaji hao, kwa maana hiyo tatizo lilikuwa ni mwalimu aliyepita ( Salum Bausi. Nimewatazama wachezaji hao na nimeridhika kuwa wanaweza kuisaidia Zanzibar hivyo hakukuwa na sababu yoyote ya kutowaita, hata chama cha soka ( ZFA) walijua kuwa nitawaita kwa kuwa tayari niliwaambia nitafanya hivyo"

Kuachwa kwa wachezaji hao mwaka jana kulipigiwa kelele nyingi na wadau wa soka nchini, si Visiwani tu, bali pia hata wale wa upande wa Bara walishangazwa kuachwa kwa wachezaji hao ' roho' ya safu za ulinzi katika klabu zao za Yanga na Azam.; "

Morocco amewaita wachezaji kadhaa wazoefu katika kikosi hicho akiwemo kiungo wa Sofa Paka ya Kenya, Abduhalim Humud, pia wachezaji kama Suleimani Kassim, Amir Omary, Hamis Mchana ambao wanafanya vizuri katika ligi kuu ya Bara wameitwa katika kikosi; " Mimi sikuangilia sababu zisizo za kimpira, nilitazama ni wachezaji gani ambao wanaweza kuisaidia Zanzibar. Nimeangali uwezo wao katika siku za karibuni, upeo wao katika timu ya Taifa" anasema Morocco kocha wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, na JKT Oljoro.



Comments