MASHAUZI CLASSC NDANI YA BAGAMOYO JUMAMOSI HII …ni mambo ya Sura Surambi



MASHAUZI CLASSC NDANI YA BAGAMOYO JUMAMOSI HII …ni mambo ya Sura Surambi
MASHAUZI CLASSC NDANI YA BAGAMOYO JUMAMOSI HII …ni mambo            ya Sura Surambi

KWA mara nyingine tena, wakazi wa Bagamoyo wanapelekewa ile kitu roho yao inataka – Ni kundi zima la Mashauzi Classic Modern Taarab chini yake Isha Mashauzi.

Kundi hilo Jumamosi hii litajitosa katika ukumbi wa Eagles Nest kuachia burudani kali ikiwa ni sambamba na utambulisho wa nyimbo zao mpya ukiwemo Sura Surambi ambao tayari umekuwa gumzo la jiji.

Kila Mashauzi Classic wanapotia mguu Bagamoyo, hupata mapokezi mazuri na hivyo kuufanya mji huo uwe moja ya himaya zao muhimu.

Meneja wa Mashauzi Classic Suma Raga, ameiambia Saluti5 kuwa wanaendelea kuutambulisha wimbo wao wa Sura Surambi na nyinginezo kwa mashabiki wao ili kupata maoni kadhaa kabla hawajaingia studio baadae mwezi Novemba.

Wimbo wa Sura Surambi ambao umetungwa na kuimbwa na Isha Mashauzi tayari umeweza kuteka mashabiki kwenye kila kumbi wanazopiga. Kazi kwenu wakazi wa Bagamoyo Jumamosi hii.



Comments