MANCHESTER UNITED YAPONEA TUNDU LA SINDANO KWA CHELSEA …Drogba na Van Persie wafanya vitu vyao


MANCHESTER UNITED YAPONEA TUNDU LA SINDANO KWA CHELSEA …Drogba na Van Persie wafanya vitu vyao

Van Persie came close to opening the scoring for                    United in the first half

ALMANUSURA Didier Drogba apeleke kilio Manchester United baada ya kuifungia Chelsea bao lililodumu hadi dakika ya 94 kabla ya Van Persie kuchomoa na kuipa sare United katika mchezo mkali wa Ligi Kuu uliopigwa Old Trafford.

Kwa sare hiyo, Chelsea inaendelea kulinda rekodi yake ya kutofungwa msimu huu huku goli hilo la Drogba likiwa goli la 1000 la Chelsea kutinga wavuni chini kocha Jose Mourinho hususan kwenye Ligi Kuu.

Eden Hazard alipangua safu ya United akabaki yeye na kipa De Gea, akaachia shuti lilolopanguliwa na kuwa kona.

Ni katika kona hiyo iliyochongwa na Cesc Fabregas dakika ya 53 ndipo balaa lilipowasili kwa United, Drogba akausukumiza mpira wavuni kwa kichwa.

Dakika ya 90+4, beki wa Chelsea Ivanovic akalambwa kadi nyekundu baada ya kufanya faulo kwenye mstari wa hatari, baada ya hapo ukapigwa mpira wa adhabu Fellaini akapiga kichwa, kipa Courtois akapangua, mpira ukamkuta Robin van Persie aliyeujaza mpira wavuni, Old Trafford ikazizima.

 



Comments